April 2, 2016


 Mwamuzi wa mechi ya El Clasico inayosubiriwa kwa hamu kubwa leo usiku ni Alejandro Hernandez Hernandez.

 Hernandez ana umri wa miaka 33, huyu jamaa alizaliwa kuwa mwamuzi wa soka kama ambavyo umewahi kuona watu wanaonekana wamezaliwa kuwa wanasoka au wanamuziki kutokana na kuonyesha vipaji vyao mapema wakiwa watoto.


Alianza uamuzi mapema kabisa akiwa na umri wa miaka 13, akipewa nafasi ya mwamuzi msaidizi au mshika kibendera na aliifanya kazi yake vizuri kabisa.

Hernandez ameanza kuwa mwamuzi anayetambulika tokea akiwa motto, anakumbuka mara ya kwanza ilikuwa ni Juni, 993.

Ilikuwa ni mechi kati ya UD Lanzarote dhidi ya na mwenyewe anasema ilikuwa ndiyo anaanza mwanzo kabisa wa maisha aliyoyatamani kwa kipindi kirefu.

“Nilikuwa nina hofu kubwa katika mechi hiyo ya kwanza,” anaemia Hernandez.


Anasema ndoto ilikuwa ni kupata nafasi ya kuwa mwamuzi bora kabisa Hispania na duniani kote. Mwamuzi bora, lazima achezeshe El Clasico hasa kama anatokea Hispania. Ndicho atakachofanya leo mwamuzi huyo.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV