April 20, 2016


BEKI wa Kati wa Mtibwa Sugar, Andrew Vincent ‘Dante’, anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na amesema timu yoyote inayomhitaji iweke mezani shilingi milioni 50 ili ajiunge nayo.

Dante mwenye rasta ameenda mbali kwa kusema hachagui timu ya kuchezea msimu ujao iwe Mtibwa, Simba au Yanga isipokuwa yoyote itakayompa fedha anazotaka tu.


Dante amesema kwa sasa bado hajajua kama atabaki Mtibwa au la, lakini anachoangalia ni wapi kwenye maslahi ndipo atakapokwenda hata Azam FC ikiwezekana. 


“Mkataba wangu na Mtibwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu na bado sijajua kama nitabaki hapa au nitaondoka, kikubwa naangalia mwelekeo wapi ni pazuri kwangu kwa ajili ya msimu ujao.


“Kutokana na uwezo wangu na kujiamini kwangu, timu itakayonitaka inapaswa kuja na shilingi milioni 50. Kama nikiondoka Mtibwa basi msimu ujao napenda nikacheze timu moja kati ya Simba, Yanga au Azam,” alisema Dante.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV