April 5, 2016

KIIZA

Mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza na beki Juuko Murshid wamechelewa kurejea nchini kutoka Uganda kwa zaidi ya siku sita sasa.

Wachezaji hao raia wa Uganda, wamechelewa kurejea kazini jambo ambalo linaonekana kuukasirisha uongozi wa Simba.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Simba, Haji Manara amesema wamekuwa hawana mawasiliano hao.

JUUKO

“Hatuna taarifa rasmi, hakuna aliyeueleza uongozi lakini wamechelewa kwa muda wa siku sita sasa. Tunaamini si jambo jambo.

“Uongozi wa Simba unataka kuboresha nidhamu na tusingependa mambo kama haya yawe yanajitokeza,” alisema.


Taarifa zinasema wachezaji hao wamekuwa hawapokei namba za viongozi wa Simba kw amakusudi jambo ambalo linaonyesha wanachofanya walikusudia.

2 COMMENTS:

  1. Kwa Simba hata wakirudi hamtawafanya kitu kwa kuwa ni wachezaji wa kigeni,kwa ujumla SIMBA nidhamu ni sifuri,
    nidhamu iko AZAM na YANGA.Wanaochukuliwa hatua kali mara nyingi ni wazawa,Tuwe wakweli.

    ReplyDelete
  2. Ngoja tusubiri tuone nini watafanywa.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV