April 5, 2016


Kikosi cha timu ya Tanzania U17 ’Serengeti Boys’ kimeonyesha kinaweza kwa mara ya pili baada ya kuitwanga Misri kwa mabao 3-2.

Katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam, Serengeti Boys walionyesha soka safi na la ushindani.


Katika mechi ya awali, Serengeti Boys waliwatwanga Misri kwa bao 2-1, leo wakataka kujiuliza na kukutana na kipigo hicho kikubwa zaidi.

Kocha, Bakari Shime, imepata ushindi wa mabao 3-2 yaliyofungwa na Ibrahim Abdallah aliyefunga mara mbili dakika za 28, 60 na Boko Seleman aliyepasia nyavu dakika ya 36.


Mabao ya The Pharaohs yaliwekwa kimiani na mshambuliaji wake, Ahmed Saad dakika 22 pamoja na mtokea benchi, Diaa Wahid aliyefunga kwenye dakika 74.  Mechi hiyo ilikuwa na ushindani kwa pande zote mbili ambapo Serengeti wao walitawala kwenye kipindi cha kwanza huku Misri wakichukua nafasi kipindi cha pili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV