April 20, 2016

MABINGWA wa zamani wa Ligi Kuu Bara, Majimaji wamesema watahakikisha straika wao, Danny Mrwanda haondoki katika kikosi chao baada ya kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu. 

Mrwanda aliyewahi kucheza Simba na Yanga alijiunga na Majimaji mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Lipuli. 


Katibu Mkuu wa Majimaji, John Mbano ameliambia Championi Jumatano kuwa Mrwanda amekuwa msaada mkubwa kwao, yeye pamoja na mkongwe mwingine, Godfrey Taita.


“Mkataba wa Mrwanda unakwisha baada ya msimu huu kumalizika lakini hatutarajii kumuachia, amekuwa mtu muhimu kikosini kwetu na tungependa kuendelea naye msimu ujao. Tutakuwa na mazungumzo naye kwa ajili ya mkataba mpya,” alisema Mbano.Mrwanda amefunga mabao sita ambayo yameisaidia Majimaji kuwa nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 33.
SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV