April 20, 2016

Klabu ya Simba imetangaza kumfungia mchezaji wake kutocheza katika mechi tano zijazo kutokana na kile ilichodai kuwa alipata kadi nyekundu ya kizembe kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Toto Africans.

 Simba imetangaza adhabu hiyo wakati ambapo Kessy anaelekea mwisho wa mkataba wake ambao utamalizika mwishoni mwa msimu huu, ambapo pia Simba imesaliwa na mechi tano tu kumaliza mechi zote za ligi kuu msimu huu.

KESSY


Kutokana na mazingira hayo inamaanisha kuwa safari ya Kessy kuendelea kuwepo klabuni hapo itakuwa imefikia mwisho na kama hataongeza mkataba mwingine basi Wanasimba hawatamuona tena mchezaji huyo katika jezi ya Simba.

Akizungumzia suala hilo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa uamuzi huo umetokana na uongozi kurudia kutazama tukio la kadi nyekundu aliyopata Kessy alipomchezea vibaya Edward Christopha wa Toto, Jumapili iliyopita na kubaini kuwa hakucheza kiungwana.

HAJI MANARA


“Uongozi umerudia kutazama tukio la Kessy na umeamua kumfungia mechi tano licha ya kuwa alikuwa akose mechi mbili kutokana na kupewa kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyoipata.

“Kitu kingine ni kuwa alienda kuzungumza kuhusu yeye kushambuliwa na kipa wetu (Vincent Angban), tumezungumza na meneja na kocha wote hawakuripoti wala kuona tukio hilo.

KESSY AKITOKA UWANJANI BAADA YA KUPEWA KADI NYEKUNDU KATIKA MECHI DHIDI YA TOTO.


“Alitakiwa aje kuutarifu uongozi na siyo kwenda kuzungumza kwenye vyombo vya habari, uchunguzu unaendelea kubaini kama ni kweli tukio hilo lilitokea au la.

“Ikibainika kweli lilitokea basi hatua zaidi zitachukuliwa lakini kwa sasa uongozi umeamua hilo,” alisema Manara.

Katika mchezo huo wa ligi kuu dhidi ya Toto uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Simba ilifungwa bao 1-0.


1 COMMENTS:

  1. Sasa endeleeni kudai kile kichwa alichopigwa kessy na Ngoma mzunguko wa kwanza maana kazi yenu ni kulalama utafikiri wale wanaojiuza kule ohio!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic