April 4, 2016


Kocha Mkuu wa Azam, Stewart Hall, amesema kuwa Uwanja wa Chamazi, si rafiki katika mfumo wake na anatamani mchezo dhidi ya Esperance wikiendi hii ungepigwa kwenye Uwanja wa Taifa ama kwingineko.

Azam watawakaribisha Esperance ya Tunisia wikiendi hii katika mchezo wa hatua ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, kabla ya kurudia na wiki moja baadaye.

Hall, alisema mfumo wake wa kutumia mabeki watatu na kujaza viungo yaani (3-5-2) unahitaji uwanja mkubwa ili kuwaweka huru viungo wa pembeni wanaofanya kazi kama washambuliaji, lakini Chamazi ni mdogo hivyo wakati mwingine hutibua mbinu zake za mashambulizi.

“Timu za Kiarabu ndiyo mfumo wake wanapokuwa ugenini. Kwao matokeo ya suluhu ama sare yoyote ugenini ni matokeo mazuri hivyo wanakuja wakiwa na nia ya kupaki basi.”

“Inaweza kuwa ngumu kwetu kutokana na uwanja wenyewe. Ukiangalia Chamazi ndiyo uwanja mdogo pengine kuliko vyote Tanzania na katika mfumo wetu siku zote unatakiwa kuwa kwenye uwanja mkubwa ili kuwapa uhuru viungo kufanya kile unachotaka.

"Lakini mara nyingi inashindikana kutokana na uwanja kubana-hautoi nafasi kwa  Singano (Ramadhan) ama Farid Musa kuendana na mfumo.


“Naaamini kama tungekuwa na uwanja kama Taifa, Kambarage kwa mfumo wetu tungekuwa na uhakika wa kufanya makubwa zaidi,” alisema Hall.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV