April 24, 2016


Luis Suarez sasa hakamatiki baada ya kukaa kileleni kwa ufungaji bora wa mabao katika La Liga.

Suarez sasa ana mabao 34 na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye ana mabao 31, hivyo kuamsha kasi ya ugombeaji wa tuzo ya mfungaji bora ya La Liga maarufu kama Pichichi.

Suarez ameifungia Barcelona mabao manne katika mechi ambayo Barcelona imeitwanga Sporting Gijon kwa mabao 6-0.

Kabla ya hapo, Barcelona ilishinda kwa mabao 8-0 dhidi ya Derpotivo la Coruna.

Hivyo kumfanya Suarez awe amefunga mabao nane katika mechi mbili.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV