April 18, 2016

Twite

Suala la Yanga kushinda michezo yake yote mitatu ya viporo, limempa jeuri kiraka wa timu hiyo, Mnyarwanda, Mbuyu Twite na kutamka wazi kuwa ubingwa wa msimu huu ni wa kwao na hakuna wa kuwazuia tena.

Yanga ilikamilisha viporo vyake kwa matokeo ya ushindi na kuwa sawa na Azam na Simba kwa idadi ya mechi kabla ya Wekundu hao kuumana jana na Toto Africans.

Twite ametamba kuwa michezo iliyobaki ni michache na wamepanga kukomaa kuibuka na ushindi yote, hasa ukizingatia kwa sasa ameona wameanza kurejea kwenye kiwango cha juu.


"Hapa tena sidhani kama kuna timu itatukamata au kutubana huko mbele, hii ndiyo moja kwa moja mpaka ubingwa, kilichokuwa kinatupa tatizo ni hivi viporo na sasa tushamaliza, kilichobaki ni kushinda kila mechi," alisema Twite.

Purukushani katika mechi ya Simba na Toto, jana ambapo Simba ilifungwa bao 1-0

Mpaka jana kabla ya mechi ya Simba, Yanga ilikuwa kileleni kwa pointi 59, Simba 57 na Azam 55 huku kila timu ikiwa na michezo 24 na hata kama timu hizo zitafanikiwa kushinda michezo yake yote iliyobaki, Yanga itasalia kileleni kwa ponti mbili zaidi mwisho wa ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV