April 18, 2016

KIUNGO wa Yanga, Mzimbabwe, Thabani Kamusoko, amesema kwamba baada ya kuchezewa rafu kwenye goti la kulia na beki wa Mtibwa, Majaliwa Shaban, alijua hataendelea tena na atakuwa amevunjika kutokana na jinsi alivyojisikia.

Hiyo ilitokea juzi Jumamosi katika mchezo uliozikutanisha timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar na Yanga ikafanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0.


Baada ya Kamusoko kuchezewa rafu hiyo na mwamuzi Jacob Odongo kumwadhibu Majaliwa kwa kadi ya njano, kiungo huyo alionekana akitolewa nje na daktari wa Yanga, Edward Bavu huku akionekana akichechemea hali iliyosababisha kunyong'onyesha mashabiki wa Yanga kabla na baada ya muda mfupi kulipuka kwa shangwe kwa kumuona Kamusoko anarejea tena uwanjani.


Baada ya mchezo huo Kamusoko alizungumza kwa kifupi kuhusiana na rafu hiyo ambapo alikiri kuhisi ndiyo basi tena, lakini Mungu akamsaidia akarejea uwanjani.


"Dah! Nilisikia maumivu makali, kwa yalivyokuwa nilijua sitarejea uwanjani na nitakuwa labda nimevunjika lakini nashukuru Mungu akasaidia nikarudi, nipo fresh sasa hivi," alisema Kamusoko ambaye keshokutwa Jumatano anatarajiwa kuiongoza Yanga kupindua matokeo dhidi ya Al Ahly ugenini nchini Misri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic