April 4, 2016Kikosi cha Simba jana Jumapili kimeendeleza moto wake wa kufanya vizuri katika mechi zake baada ya kuitandika Nidham FC inayomilikwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) mabao 11-1.

Simba inayofundishwa na Mganda, Jackson Mayanja, ilipambana na Nidhamu FC katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ulikuwa maalum kwa Simba ambayo hivi sasa ipo katika maandalizi makali ya kujiandaa na mechi ya Kombe la FA dhidi ya Coasta Union ya Tanga itakaopigwa Aprili 11, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, lakini pia michuano ya Ligi Kuu Bara.

Mabao ya Simba katika mechi hiyo yalifungwa na Said Ndemla aliyetupia mawili, Awadhi Juma (2), Daniel Lyanga (2), Ibrahim Ajib (2) pamoja na Musa Hassan ‘Mgosi’ (2) huku lingine likifungwa na kinda wa kikosi B cha timu hiyo.

Kocha Mkuu wa Simba, Jackson Mayanja ameliambia Championi Jumatatu kuwa, pamoja na kikosi chake hicho kupata matokeo hayo bado kinatakiwa kiwe bora zaidi ya hapo.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV