April 8, 2016Mashabiki maarufu wa Al Ahly ya Misri,  Ultras Ahlawy wako jijini Dar es Salaam na wamekuwa wakifanya vurugu ile mbaya katika eneo la katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Mashabiki hao ambao wengi wao ni vijana, wamefikia Kariakoo jijini Dar es Salaam, kila jioni waaanza “amsha amsha” si mchezo.

Kuonyesha kuwa Ultras Ahlawy wako makini na kazi yao, leo wameenda kupiga mazoezi ya ushangiliaji kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Wakati timu yao inafanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja huo, wao walikuwa wakipiga tizi la kushangilia utafikiri mechi.


Yanga itakuwa kazini kwenye Uwanja wa Taifa, kesho kuwavaa Al Ahly katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika inayosubiriwa kwa hamu kuu.

1 COMMENTS:

  1. Hawana lolote, wanajaribu kuhamisha akili za wapinzani ili washinde nje ya wanja

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV