April 23, 2016SIMBA jana iliondoka kwenda kisiwani Unguja kuweka kambi ya muda kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam, huku ikimuacha kiungo wake, Mzimbabwe, Justice Majabvi.

Simba iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na pointi 57 inatarajiwa kuvaana na Azam yenye alama 55, Mei 30, mwaka huu.

Kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, ni kuwa Majabvi anasumbuliwa na maumivu ya nyama za paja ambapo anaendelea na mazoezi ya gym lakini anatarajiwa kujiunga na wenzake kesho Jumapili baada ya kumaliza program hiyo.

Aidha kwa upande mwingine, kocha wa makipa, Adam Abdallah ‘Meja’ alisema: “Tunatarajia kurudi siku moja kabla ya mchezo. Tumeamua kuweka kambi huko kwa kuwa ni sehemu tulivu kwa wachezaji hivyo tunaamini itasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuwakabili Azam.”

Raundi ya kwanza timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2, mabao ya Simba yalifungwa na Ibrahim Ajib huku John Bocco, akiifungia pia Azam mabao mawili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV