April 19, 2016Na Saleh Ally, Coruna
Washindi wa “Kwea Pipa Kwenda Spain na Azam Sports HD” wamekuwa Watanzania pekee na wa kwanza kuligusa benchi ambalo kesho wachezaji wa Barcelona na kocha wao, Luis Enrique watakaa wakati timu hiyo ikiivaa Derpotivo La Coruna kwenye Uwanja wa Raizor mjini hapa.

Washindi Ismail Salim na Jamal Mussa wamefaya ziara kwenye uwanja huo wakiongozana na washindi wengine kutoka Hong Kong na Sweden na wao pekee ndiyo waliligusa benchi hilo.

Benchi hilo lilikuwa limefunikwa na si ruhusa mtu kukaa. Lakini Watanzania hao wakasogea na kupiga picha, hakuna anayeweza kukataa kwamba wameligusa hata kabla ya Enrique kesho.

Washindi hao watakuwa uwanjani hapo wakishuhudia mechi hiyo inayotarajiwa kuwa kali kwelikweli.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV