April 27, 2016

Mwamuzi anamaliza mchezo, Yanga 2, Mgambo 1

Dakika ya 90+2

Dakika ya 90+1: Yanga wanashambuliwa.

Dakika ya 90. Zimeongezwa dakika mbili za nyongeza.

Dakika ya 89: Mchezo unaendelea.

Dakika ya 86: Yanga wanapata kona, Kaseke anapiga lakini kipa anaokoa.

Dakika ya 84: Mgambo wanamiliki mpira kwa dakika moja sasa.

Dakika ya 82: Yanga wanaongoza mabao 2-1, Tambwe ameshindwa kutumia nafasi ya wazi ya kufunga bao.

Dakika ya 79: Mgambo wanafanya mabadiliko, anatoka Nassor Gumbo anaingia Ally Nassor.
 

Dakika ya 73: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Niyonzima anaingia Thaban Kamusoko.

Kaseke anaipatia Yanga bao la pili baada ya kutokea piga nikupige katika lango la Mgambo, mpira ukamkuta Kaseke akiwa mwenyewe, akapiga shuti kali na kuwa bao la pili kwa Yanga na kwake pia katika mchezo wa leo.

Dakika ya 71: Kasekeeeeeee
 
Dakika ya 63: Kamusoko ambaye leo yuko benchi anapasha misuli.

Dakika ya 60: Mgambo wanapata faulo nje ya eneo la 18, wanapiga lakini inashindwa kuwa na faida.

Dakika ya 55: Mgambo wanafanya mashambulizi ya nguvu lakini wanashindwa kutumia nafasi.

Dakika ya 50: Ngoma tena anakosa bao la wazi baada ya kupewa pasi na Tambwe, tayari Ngoma alishaanza kushangilia akijua mpira unaingia wavuni.

Dakika ya 47: Ngoma anashindwa kumalizia mpira uliokuwa ukipita mbele kidogo ya lango la Mgambo.

Dakika ya 45: Yanga wanafanya mabadiliko ametoka Paul Nonga, ameingia Donald Ngoma.

Kipindi cha pili kimeanza

Mpira ni mapumziko

Dakika ya 45: Yanga wanafanya shambulizi la nguvu lakini Simon Msuva anashindwa kumalizia mpira.

Dakika ya 44: Kiungo Deusi Kaseke anaisawazishia Yanga kwa kuumalizia mpira uliopigwa kwa kichwa na Amiss Tambwe kutoka upande wa kulia, mabeki wa Mgambo wanabaki wanatazamana.

Kasekeeeeeeeee

Dakika ya 37: Mchezo unaendelea
 
Dakika ya 35: Mchezo umesimama, kipa wa Mgambo kaumia.

Dakika ya 34: Mvua imekatika, timu zote zinashambuliana kwa zamu, mpira umemilikiwa zaidi na viungo wa timu zote.
 

Dakika ya 30: Msuva anakatwa ndani ya eneo la hatari la Mgambo lakini mwamuzi anapeta.

Dakika ya 27: Salum Telela anapewa kadi ya njano kutokana na kucheza faulo.

Dakika ya 26: Mgambo wanaendelea kuwa wagumu kukubali ngome yao kupitika.

Dakika ya 23: Mchezo unaendelea.

Juma Abdul ilionyesha kuwa na maumivu na alitoka akiwa anachechemea.

Dakika ya 21: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Juma Abdul anaingia Mbuyu Twite.

Dakika ya 21: Kipa wa Mgambo, Said Hamis ameumia na yupo chini, mchezo umesimama.

Dakika ya 19: Mgambo wanafanya shambulizi lakini inakuwa offside.

Dakika ya 15: Mgambo wanazuia vizuri lango lao kutokana na Yanga kuonekana kutafuta bao kwa nguvu.

Dakika ya 10: Yanga wameamka na kuanza kushambulia lango la Mgambo. 

Bao hilo limefungwa dakika ya 4, mfungaji ni Bolly Ajaly

Dida alimuanzishia mpira Telela ambaye alishindwa kuumiliki na kujikuta akinyang'anywa na washambuliaji wa Mgambo ambao walitumia nafasi hiyo kutupia mpira wavuni

Mgambo wanapata bao kutokana na uzembe wa kiungo wa Yanga, Salum Telela.


Dakika ya 3: Timu zote zinacheza mchezo wa kusomana, mchezo bado haujachangamka.


Mchezo umeanza


Timu ndiyo zinaingia uwanjani kwa ajili ya kuanza mchezo.


Idadi ya watu siyo wengi sana uwanjani kutokana na mvua kunyesha jijini Dar es Salaam, mpaka sasa kuna manyunyu eneo hili la Uwanja wa Taifa.


KIKOSI CHA YANGA:
Deogratius Munish ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Paul Nonga, Amissi Tambwe, Deus Kaseke.

WANAOANZIA BENCHI
Benedict Tinocco, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Matheo Anthony, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Mwinyi Hajji.

 
KIKOSI CHA MGAMBO:
Said Hamis, Salum Mlima, Chande Magonja, Henry Chacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Nassor Gumbo, Mohammed Samatta, Herbert Lukindo, Bolly Ajaly, Salum Gila.

WANAOANZIA BENCHI
Mudathir Hamis, Bushiru Mohammed, Francis, Anyosisye, Ally Nassoro, Nurdin Mkomeni, Uda Bakari, Abuu Daud.


Timu zote zimeshaingia uwanjani kupasha misuli, wachezaji wote watakaoanza na wale wanaoanzia benchi.

1 COMMENTS:

  1. YANGA BWANA,KWELI ANAEJUA ANAJUA TU MAANA HATA WAKITANGULIWA KUFUNGWA HAWANA KUKATA TAMAA.KWA UJUMLA YANGA WANA BONGE LA MWALIMU,WASIMUACHE.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic