April 27, 2016

Wakati Yanga ikipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, upande mwingine wa jiji hilo, Azam FC nayo imeichapa Majimaji mabao 2-0.

 


   Ushindi huo wa timu zote mbili unamaanisha kuwa Yanga imeendelea kujikita kileleni wakati Azam imeishusha Simba na sasa Azam ndiyo inashika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara.

  Azam ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex, ilipata ushindi huo kutokana na mabao yaliyofungwa na Mudathir Yahya.  



  Mudathir ambayeni kiungo alifunga mabao hayo katika dakika ya 51 na 63, hivyo kuiwezesha Azam kufikisha pointi 58 katika michezo 25 huku Yanga ikiongoza kwa kuwa na pointi 62 katika michezo 25 pia. Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 57 katika michezo 25.

Kikosi cha Azam FC ambacho kilianza katika mchezo huo wa leo ni hiki hapa:

1 Aishi Manula
2. Erasto Nyoni
3. Gadiel Michael
4. David Mwantika
5. Aggrey Morris
6. Jean Mugiraneza
7. Ramadhan Singano
8. Mudathir Yahya
9. Salum Abubakar (C)
10. Didier Kavumbagu
11. Khamis Mcha

Walioanzia benchi:
Ivo Mapunda
Said Morad
Abdallah Kheri
John Bocco
Ame Ally
Shabaan Idd
Abdallah Masoud



2 COMMENTS:

  1. Tunashukuru kwa habari nzr unazotupatia Ila tunakosa, fixtures na misimamo ya ligi tofauti tofauti ikiwemo ya kwetu hapa nyumbani. Leo unatuambia Azam imemshusha simba Ila table haipo.

    ReplyDelete
  2. Tunashukuru kwa habari nzr unazotupatia Ila tunakosa, fixtures na misimamo ya ligi tofauti tofauti ikiwemo ya kwetu hapa nyumbani. Leo unatuambia Azam imemshusha simba Ila table haipo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic