May 8, 2016


Azam FC imeifunga kwa Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Ushindi huo unairejesha Azam FC katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya Simba kupoteza kwa kuchapwa bao 1-0 na Mwadui FC, leo.

Kwani Azam FC imefikisha 70 baada ya kucheza mechi 28 na Simba inaendelea kubaki na pointi 68 ikiwa na mechi 27.

Tayari bingwa wa Bara ameishapatikana ambaye ni Yanga na sasa itakuwa ni vita ya Azam na Simba kuwania nafasi ya pili ambayo ni kama heshima tu au wingi wa fedha kutoka Vodacom.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV