May 8, 2016


Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amemtangaza kuwa kocha bora wa Tanzania.

Julio amesema hayo mara tu baada ya mechi kati yao dhidi ya Simba kwisha na Mwadui FC kushinda kwa bao 1-0.

“Mimi ndiye kocha bora hapa Tanzania. Nilitaka sana kuifunga Simba ili kuwaonyeshea kuwa mimi ninaweza kuwafunga kwa kuwa nina uwezo.

“Hawa Simba walitufukuza mimi na kocha Kibadeni, hii ni laana yetu kwa kuwa nilianza kumfunga kocha wao wa zamani (Patrick Liewig wa Stand United). Leo nimewafunga tena leo kupitia kocha wao sijui nani, sijui Mayanja.

“Nataka wajue makocha wazalendo pia wanapaswa kuthaminiwa. Waache mambo yao ya kizamani kuwa wanaona makocha wazalendo hawana maana. Waache majungu, waache kutudharau,” alisema Julio akionyesha kujiamini.


KIkosi cha Mwadui kilionyesha soka safi na kuizidi Simba ambayo licha ya kucheza vizuri lakini ilishindwa kuonyesha kuwa ingeifunga Mwadui FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV