May 5, 2016Uongozi wa klabu ya Azam FC, umesema kocha wao, Stewart Hall bado anaendelea kuitumikia klabu hiyo na taarifa za kwamba ameijiuzulu, hazina ukweli.

Taarifa zimekuwa zikizagaa mitandaoni kwa kasi kubwa kwamba Hall raia wa Uingereza ameamua kuachia ngazi baada ya kumtumia beki Erasto Nyoni aliyekuwa na kadi tatu za njano.

TFF imetangaza uamuzi wa kuipoka Azam FC pointi tatu baada ya kumchezesha Nyoni katika mechi dhidi ya Mbeya City.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema taarifa zinazoenea mitandaoni kwamba kocha huyo amejiuzulu, si za kweli.

“Kocha Hall bado tunaye, habari za kwamba amejiuzulu si za kweli kabisa. Hili suala lipo ndani ya klabu, tutakaa na kulijadili na baada ya hapo tutalizungumzia,” alisema Kawemba.


Suala la Nyoni kucheza akiwa na kadi tatu za njano, limeonekana kuwashangaza wadau wengi wa soka kwa kuwa waliamini Azam FC ni moja ya timu au kikosi makini kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV