May 5, 2016


Takribani saa 14 tu baada ya mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi Chapwe kutangaza nia yake ya kuwania Urais wa DR Congo, askari wa jeshi la nchi hiyo wameizunguka nyumba yake anayoishi.

TP Mazembe ndiyo timu aliyochezea Mtanzania, Mbwana Samatta na kupata jina kubwa kabla ya kujiunga na KRC Genk ya Ubeligiji. Lakini bado Mtanzania, Thomas Ulimwengu anaendelea kuichezea timu hiyo.


Taarifa zimeeleza, Serikali ya DR Congo imetoa kigali cha kukamatwa kwa Katumbi kwa maelezo kwamba amekuwa akikiuka mambo kadhaa na tayari wizara ya ulinzi ya DR Congo imesema inataka afunguliwe mashitaka.

Hata hivyo kumekuwa na taarifa za kutaka kumbana Katumbi ikielezwa Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambacho ni kirefu cha DR Congo anaonekana kutofurahishwa na hilo.

Katumbi ambaye anaaminika kwa sasa ndiye Mkongo maarufu kuliko wote duniani, amekuwa presha kubwa kwa Rais Kabila.


Bado haijaelezwa mwisho wa askari hao wa DR Congo, lakini taarifa nyingine zimesema Katumbi analindwa na askari kutoka Marekani na Afrika Kusini ambao wana mafunzo ya juu kabisa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV