May 9, 2016

WEMA
Baada ya Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya  Sagrada Esperanca ya Angola, msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, amefunguka kuwa hajui ni kwa nini amekuwa akimpenda kiungo wa timu hiyo, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima.

Katika mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Wema ambaye pia alikuwa Miss Tanzanani mwaka 2006, akiwa amekaa Jukwaa la VIP A kwa ajili ya kutoa sapoti kwa timu yake hiyo.

NIYONZIMA
Wema alisema kuwa upendo wake kwa kiungo huyo ni mkubwa mno kiasi kwamba hajui kwa nini inakuwa hivyo, lakini akaongeza kuwa inawezekana kuwa ni kutokana na uwezo wake anaouonyesha uwanjani ambapo katika mchezo huyo aliwapa wakati mgumu viungo wa Esperanca.

“Mimi ni shabiki wa Yanga damu kabisa, tangu nazaliwa na utabiri wangu umeenda vizuri, maana nilisema kabla ya mchezo kuwa tutashinda na imekuwa kweli, ushindi huo ni mzuri kwetu maana nilikuwa na hofu kama tungeshinda bao moja pekee huenda ingekuwa tatizo kwa upande wetu.

“Kiukweli nampenda Niyonzima kila siku na sijui kwa nini, pia  leo (juzi) amefanya vizuri kwa kuhakikisha tunapata ushindi kabla ya mchezo wa marudiano na naamini watafanya vizuri kwa kufuzu hatua inayofuata, muhimu ni kuwaombea tu,” alisema Wema.  0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV