May 26, 2016


Wakati wengi waliamini baada ya Newcastle United kuteremka daraja, Kocha Rafa Benitez angetimua zake, mambo yamekuwa tofauti.

Benitez amesema ataendelea kubaki Newcastle na kupambana kuirejesha Ligi Kuu England.

Benitez raia wa Hispania ni kocha mkubwa, amepita timu kubwa kama Liverpool, Inter Milan na Real Madrid. Ndiyo maana watu wengi waliamini angeondoka.

Lakini ameweka msisitizo kuwa anaendelea kubaki kuwa kocha wa Newcastle pale St James Park.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic