May 29, 2016



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amewashangaa watu ambao wamekuwa wakijitokeza kuwavamia au kuwalaumu viongozi wa Simba ambao wanatoa kila kitu kadiri ya uwezo wao kuhakikisha timu inafanya vizuri.

Kama hiyo haitoshi, Hans Poppe amesema, beki Hassan Kessy ambaye ameondoka Simba na kujiunga Yanga, waziwazi aliwasaliti.

“Viongozi hawachezi pale uwanjani, kawaida wanafanya kila kitu kuhakikisha wachezaji wanapata na kwenda kucheza.

“Wao ndiyo wanatakiwa kuwa na moyo na klabu, wawe na huruma na mashabiki. Lakini si mtu anapewa kadi nyekundu kwa makusudi kabisa, halafu ,mashabiki wanavamia viongozi.

“Wakati mwingine nanyama kwa kuwa ukibishana na wajinga na wewe utaonekana ni mjinga. Lakini angalia alichokifanya Kessy, kadi nyekundu katika mechi dhidi ya Toto ambayo inaonyesha huyu alipania kuipata.

“Siku chache baadaye anajiunga na timu nyingine, tena kukiwa na tetesi nyingi kuhusiana na ushiriki wake nao. Sasa unataka nini tena uone kama wewe ni shabiki ili kujua tatizo liko kwa nani?” alihoji.


Hans Poppe amesisitiza msimu ujao, wanalazimika kuwa makini sana ili kuepuka wachezaji ambao wanaingia Simba kwa lengo la usaliti.

2 COMMENTS:

  1. Tatizo la simba ni kumpa madaraka mtu aliyeteuliwa na Aveva kuwa msemaji na mkubwa wa timu tofauti na wale waliochaguliwa na wanachama.Simba itaendelea kufeli hadi pale watapowaheshimu wanachama wao waliowaweka madarakani na si kuwaita wajinga kama afanyavyo huyo Poppe

    ReplyDelete
  2. Ama kweli Simba hakuna nidhamu kuanzia viongozi mpaka wachezaji,UNAMWITAJE MWANACHAMA WAKO MJINGA?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic