May 29, 2016



Aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage ameshindilia msumari kwa uongozi wa sasa wa Simba na kusema walichemsha kumuacha mshambuliaji Amissi Tambwe huku akichambua tofauti yake na yule aliye Simba sasa Hamisi Kiiza.

Rage amesema Tambwe hakupaswa kuachwa, na kusisitiza, ana tofauti kubwa na Kiiza.

“Tambwe ni mzuri katika ufungaji. Lakini ana nidhamu ya juu kabisa ndani na nje ya uwanja. Ni mchezaji ambaye hana usumbufu na anaijua kazi yake, Yanga wamepata mtu.

“Lakini Kiiza namuona ana upungufu mkubwa ndani na nje ya uwanja hasa katika suala la nidhamu. Hapa Simba walikosea kwa kweli ingawa sijui nini kilitokea,” alisema Rage alipozungumza na Radio One.

Tambwe raia wa Burundi ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara baada ya kufunga mabao 21 akimuacha Kiiza kutoka Uganda aliyefunga 19 na kukaa kileleni kwa muda mrefu.

Rage alisisitiza kuwa Simba wanapaswa kuwa makini sana katika suala la usajili ili kurejesha nguvu na heshima ya Simba.

Uongozi wa Rage ulifeni katika misimu miwili ya mwisho na uongozi uliochukua nafasi wa Evans Aveva pia umefeli misimu miwili ya mwanzo, hivyo kuifanya Simba idorore kwa misimu minne mfululizo.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alieleza uamuzi wake wa kusitiza kumpa gari Kiiza kama alivyoahidi akielezwa kuudhika na utovu wa nidhamu aliouonyesha hatua za mwisho za ligi.

Pia alizungumzia suala la Tambwe na kusisitiza: "Hili suala nimelizungumza sana, sijui kipi kinawafanya watu wawe wanalipindua na kuuliza tena. Kocha wa wakati ule (Patrick Phiri) hakuwa akimtumia, tukaona tutaua kipaji chake tumuache aende. Lakini ajabu kabisa, watu wanarudia tena na tena, sijui kwa nini wanalipenda sana jambo hili."


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic