May 28, 2016

TSHABALALA (KUSHOTO)...

Simba imeionya Yanga kutothubutu kumlaghai beki wake wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ kwa kutaka kung’ang’aniza kumsajili kwani bado ana mkataba wa mwaka mmoja.

Taarifa zinasema, baadhi ya wapenzi wa Yanga wamekuwa wakiendesha harakati za chinichini kumsajili Tshabalala kisha kuibua madai ya kuwa amemaliza mkataba ili baadaye achezee timu yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe, amezungumza na Salehjembe na kusema:

“Kwanza Tshabalala anajitambua, hivyo hawataweza kufanikiwa, halafu safari hii hatutakubali kufanyiwa mambo yasiyofaa kwani wote tunajua mchezaji huyu ana mwaka mmoja katika mkataba wake.

HANS POPPE
“Kama Yanga wanataka kweli kumsajili basi waje tuzungumze kuliko kutaka kufanya mambo ya kijanja, haitakuwa jambo jema, pia tumejipanga Simba kutokubali kuonewa.

"TFF wamekuwa wakifanya mambo yao hovyo kabisa, hawa ndiyo wanasababisha hata watu kuona kila kitu cha ujanja kinawezekana. Hasa zile kamati zao ndiyo chanzo cha matatizo mengi.

"Kamati zinaendeshwa kishabiki, watu ni wale wanaojua kila kitu lakini wanapindisha sheria makusudi kwa kuwa wanajua hakuna wa kuwafanya kitu, hii ni dhuluma kubwa katika soka na Simba hatuwezi kukubali tena kutokea kwa kwa suala kama lile la Singano," alisisitiza Hans Poppe.

Msimu uliopita, Simba ilimpoteza winga wake Ramadhani Singano ambaye mkataba ulielezwa kumalizika na baadaye akajiunga na Azam FC lakini hadi leo kesi hiyo haijaisha TFF na Singano anaendelea na maisha yake na Azam FC. 

1 COMMENTS:

  1. Hizo ni siasa tu ili kulaghai mashabiki wa simba, tengenezeni kikosi bora kama timu imewashinda basi achieni ngazi. Mbona mlipopewa Okwi hamkusema kuna ujanja ujanja!? ila kwa Singano mnalalamika wakati nyie ndo mlitaka kumdhulumu dogo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic