MAGURI |
Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema msimu ujao lazima mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguri, awe mchezaji wake na anaamini atafanya mambo mengi makubwa.
Maguri ambaye anashika nafasi ya nne kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 15, mara kadhaa amekaririwa akisema kuwa hana furaha ndani ya timu hiyo.
Julio alisema: “Nataka kumsajili Maguri, kwanza ni mchezaji mzuri pia nataka kukilinda kiwango chake ambacho naona kuna watu wanataka kukiua.”
Pamoja na kufunga mabao hayo lakini Maguri amekuwa hana uhusiano mzuri na kocha mkorofi, Patrick Liewig ambaye falsafa yake ilikuwa ni chanzo cha kuporomoka kwa Simba.
Liewig ndiye aliyewaondoa wachezaji wote wakongwe waliokuwa Simba na kuamuamini vijana ambao wamekuwa tatizo badala ya mafanikio Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment