May 14, 2016

MAYANJA

Bosi wa benchi la ufundi la Simba, Jackson Mayanja amesema licha ya kuwa na wachezaji wengi wa kikosi cha pili, atahakikisha wanaifunga Mtibwa Sugar, kesho katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mayanja ambaye ni raia wa Uganda amesema ataingia uwanjani bila ya nyota wake wengi wa kigeni ambao wamegoma kutokana na kucheleweshewa mishahara yao.

“Kutokana na kikosi tulichokuwa nacho sasa tunaangalia jinsi ya kupambana na kushinda michezo yote iliyosalia, tunaanza na Mtibwa Sugar halafu JKT Ruvu.

“Tunaamini tutafanya vizuri japo hatutakuwa na wachezaji wengi wa kikosi cha kwanza,” alisema Mayanja ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi huu.

Kocha wa Mtibwa, Mecky Maxime akizungumzia mchezo huo, alisema: “Maandalizi yanaendelea vizuri na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri sina majeruhi na naahidi kuifunga Simba kwani nataka tushinde mechi zote za mwisho.” 


Mara ya mwisho Simba kupata ushindi kwenye ligi kuu ilikuwa ni Machi 19, mwaka huu baada ya kuifunga Coastal Union mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic