May 8, 2016


-KADI NYEKUNDU Ajib analambwa kadi nyekundu baada ya kumrukia kwa makusudi Kabunda

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 90, Mgosi anaingia vizuri na kutoa krosi nzuri lakini Mobby anaokoa vizuri kabisa
SUB Dk 89, Salim Khamisi anaingia kuchukua nafasi ya Sabato kwa upande wa Mwadui
 KADI Dk 86 Majegwa analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Mnyate
SUB Dk 85, Simba wanamtoa Kiiza na nafasi yake inachukuliwa na Mussa Hassan Mgosi
 Dk 81 hadi 84 Mwadui wanaonekana kuuthibiti zaidi mpira hasa katika eneo lao huku wakijaza wachezaji wengi zaidi katika ukabaji
Dk 80, Majegwa anapiga krosi nyingine lakini inaishia kwa mabeki wa Mwadui
Dk 77, Simba wanapoteza nafasi baada ya shuti la Ndemla kutoka nje sentimeta chache
Dk 76, Mrope anaingia vizuri na kupiga mrosi kwa Mnyate, naye anatelezesha kichwa lakini mpira unawahiwa na mabeki MWadui wanaokoa

GOOOOOOOOOOOOO Dk 73 Jamal Mnyate anawachambua mabeki wa Simba kama karanga na kupiga shuti la kifundi kabisa pembeni mwa lango.....
Dk 71 Mnyate anaingia vizuri, anapiga shuti lakini lufunga anaokoa na kuwa kona. Jabir Aziz 'Stima' anachonga kona matata kabisa, kipa Agbani anaokoa na kuwa kona tena. Inachongwa tena lakini inaokolewa
 SUB Dk 69, Mwadui wanamtoa Mandawa na nafasi yake inachukuliwa na Julius Mrope
Dk 69, Kiiza anatoa krosi nzuri lakini Ndemla anauuinua na kushindwa kuudhibiti
DK 67, Mandawa anaruka na kutuliza vizuri kabisa lakini anakosa balansi na Simba wanauchukua kwa ulaini kabisa
Dk 65, Kiiza anaruka na kupiga kichwa cha kuchupa, mpira unatoka nje
Dk 64, Majegwa anapiga krosi nzuri kabisa, lakini Kiiza anaanguka mwenyewe
Dk 60, inachongwa kona safi kabisa Majabvi anaunganisha lakini mpira mkuubwaaaaa

Dk 58, Majwega anapiga kona, inakuwa kona tena. Anapiga nyingine, hii ni hovyo kabisa
Dk 56, Simba wanafanya shambulizi jingine lakini mabeki wa Mwadui wanaonekana wako makini mipira ya juu
Dk 52 Kiiza anunganisha mpira wa kichwa lakini mpira unamgonga na kutoka nje
Dk 49 Mandawa anajaribu shuti kali lakini linatoka nje. Hata hivyo mwamuzi msaidizi anasema ilikuwa offside
Dk 46 kipindi cha pili kimeanza, Mwadyi FC wanaonekana kumiliki zaidi mpira lakini wanacheza chini, yaani u[ande wa lango lao
SUB Dk 46, Simba wanawatoa Ugando na Mwalyanzi na nafasi zao zinachukuliwa na Majegwa na Ajib

MAPUMZIKO
DAKIKA 3+ ZA NYONGEZA
Dk 44, krosi safi ya Mwadui, lakini mabeki Simba wanapambana kuokoa
Dk 41, Mwadui FC wanapata kona, inachongwa na Luhende lakini kipa anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 40, Mandawa anaachia bunduki hapa, lakini kipa Agbani anafanya  kazi ya ziada kuokoa
KADI Dk 40, Kazimoto analambwa kadi ya njano kwa kucheza madhambi
Dk 39, Kiiza anapoteza nafasi kubwa zaid ya Simba hadi sasa. Beki anaanguka, anabaki yeye na kipa, pamoja na kwamba anamuona Mobby anakwenda kulinda lango, yeye anapiga tu hivyohivyo, beki huyo anaokoa kwa ulaini kabisa
Dk 36 hadi 38, mpira zaidi mpira unahamia katikati kila timu ikigonga pasi nyingi

Dk 35, Simba wanapoteza nafasi nyingine, Ugando anaingia vizuri lakini anakuwa hana mawasiliano na wnzake baada ya kupiga krosi inayokosa mtu
Dk 33, Mnyate anapata mpira mzuri karibu na lango la Simba, lakini anapiga shuti dhaifu ambalo halijalenga lango
Dk 30, Nimuboma anapiga krosi nzuri lakini Mwadui wanaokoa na kuwa kona isiyo na faida
Dk 29, krosi nzuri ya Tshabalala, Kiiza anaunganisha lakini anapaisha
Dk 28, shambulizi jingine kali la Simba, Kiiza anapiga krosi nzuri. Ndemla anaunganisha lakini kipa anaokoa, beki naye anaosha
Dk 25, Mandawa tena anapoteza nafasi nyingne kwa kupiga shuti na kupaisha buuu

DK 24, Ndemla anaingia vizuri na kujaribu kwa mguu wa kushoto, shuti ni kubwa lakini halijalenga lango
Dk 21, Mwadui wanapoteza nafasi nzuri baada ya krosi nzuri ya Mnyate lakini Mandawa anafanya uzembe na kupaisha puuuuu
SUB Dk 19, Kado anatolewa baada ya kuumia. Nafasi yake inachukuliwa na Jackson Abdulrazak
Dk 15, krosi safi kabisa na Nimuboma, Kiiza ajaribu kuiwahi lakini Kado anaruka vizuri na kuokoa vizuri kabisa
Dk 13, Beki Juuko Murshid anamtwanga kiwiko Kelvin Sabato, yuko chini anagaragara. Bahati nzuri kwake waamuzi hawakuona. Hakika si kitu kizuri sana katika mchezo wa soka

Dk 10, Beki Iddy Mobby anaokoa mpira unaoonekana kama ulivuka msitari lakini mwamuzi anasema laaa! Haukuwa uevuka...
Dk 9, krosi safi ya kwanza kwa Mwadui FC, lakini anaruka na kushindwa kupiga vizuri
Dk 6 hadi 8 Mwadui FC wanaonekana kumiliki mpira vizuri kuliko Simba
Dk 5, Mwalyanzi anaingia vizuri, anagongwa na kuanguka. Mwamuzi anasema twende...
Dk 3, Simba nao wanaonekana kuchangamka na kugongena vizuri hadi lango mwa MWadui. Bado hakuna hatari kubw ahadi sasa
Dk 1 Mechi imeanza kwa kasi kidogo na Mwadui FC wakionekana kuwa kasi wakigongeana vizuri na kuwapa presha Simba

5 COMMENTS:

 1. Duh mwaka wa njaa msimbazi. Kweli mwadui kawa kama chelsea kwa totenham..... Let's call it a season..... Jipangeni kwa msimu mwingine meeeen...

  ReplyDelete
 2. Simba hawana wa kumlaumu zaidi yao wenyewe.Walitumia muda na nguvu nyingi kuilazimisha TFF izipangie Yanga na Azam mechi mfululizo za viporo na Simba ipumzike kuzisubiri zimalize viporo.Tangu hapo Simba haijashinda tena,imepoteza mechi mbili na kwenda sare moja katika ligi kuu ya Vodacom na kufungwa na Coastal Union 2-1 kombe la shirikisho.Mechi zote nne zimefanyika uwanja wa Taifa.Katika mechi zao tatu za ligi kuu haijafunga hata goli moja

  ReplyDelete
 3. Kwa mwaka huu Yanga walijiandaa vizuri zaidi.Wameweza kuzifunga timu 14 kati ya 15 walizotakiwa kucheza nazo katika ligi kuu ya Vodacom,aidha mechi moja au zote mbili nyumbani na ugenini kama ilivyofanya kwa Simba sc.ni Azam pekee ndiyo imepona kipigo toka kwa Yanga.Halafu Donald Ngoma ameweza kuzifunga magoli timu 11 kati ya timu 15 zilizocheza na Ynga katika ligi hii.Kumbuka kwamba amezifunga timu zote zilizoko top 5 yaani Azam,Simba,Mtibwa na Mwadui.Kwa upande wa Tambwe yeye amezifunga timu 9 kati ya 15 za ligi kuu zilizocheza na Yanga

  ReplyDelete
 4. Kama Kesy alifungiwa kwa kucheza rafu na kupewa kadi nyekundu,tunasubiri tena Hajj Manara aje na uamuzi waliofikia kuhusu Ajib ambaye alimrukia kwa makusudi Kabunda na kusababishwa kupewa kadi nyekundu!

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV