May 8, 2016Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za rambi rambi kwa Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya (MREFA) kutokana na kifo cha Mweka Hazina wa chama hicho, Emmanuel Kavenga kilichotokea jana mchana katika Hospital ya Rufaa ya Mbeya.Katika salamu zake, Malinzi amewapa pole familia ya marehemu Kavenga, ndugu, jamaa, marafiki na MREFA na kusema kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchin, TFF ipo pamoja nao katika kipindi hichi kigumu cha maombolezo.


Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa marehemu Block T, Mbeya na kwamba mwili wa marehemu Kavenga unatarajiwa kusafirishwa kesho Jumatatu Mei 9, 2016 kwenda Dodoma, ambapo mazishi yanatarajiwa kufanyika Jumatano, Mei 11, 2016 katika mji wa Mpwapwa mkoani humo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV