May 7, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA
-Yanga wanazidi kushambulia kwa nguvu tena kuhakikisha wanapata bao, lakini Sagrada wamerudi nyuma na kuendelea kufanya ulinzi mkali
GOOOOOOOO Dk 90+1 Matheo Anthony anageuka na kupiga shuti laki la kushituka bila ya kutegemea. mpira unamgusa Antonio Kasule na mpira kujaa wavuni

DAKIKA 3 ZA NYONGEZADk 89 Yanga wanaendelea kugongeana vizuri lakini Sagrada wote wamerudi nyuma
Dk 88, Niyonzima, Matheo na Tambwe wanagongeana vizuri lakini mwisho pasi nzuri ya Niyonzima, Tambwe na Msuva wanategeana
Dk 86, Matheo Anthony ndani ya eneo la hatari akiwa katika nafasi nzuri baada ya kupokea pasi nzuri ya Tambwe lakini anashindwa kufunga na kupoteza nafasi nzuri kabisa kwa Yanga

Dk 84, Niyonzima anaingia vizuri na kupiga krosi safi kabisa, lakini Mwashiuya anapiga shuti hooooovyooo kabisa
DK 81 Morais anamzuia Mwashiuya na mwamuzi anasema ni faulo, inachongwa vizuri lakini mpira unaokolewa vizuri kabisa na Chisola

Dk 80 Chisola anapiga krosi hatari kabisa lakini Cannavaro anakuwa mjanja, anaruka na kuokoa mpira huo
Dk 79 Yanga wanaonekana kushambulia zaidi na kasi yao inaonekana kuwashinda Esperanca
Dk 75 hadi 78, Esparanca wanaonekana kupoteza muda mwingi

Dk 74, Yanga wanafanya shambulizi kali kabisa kwa kipindi cha pili baada ya shuti la Mwashiuya kuokolea, ukamkuta Joshua naye akaachia shuti kali lakini wanaokoa hapa Esperanca
Dk 73, krosi nzuri ya Twite inakosa mtu na mabeki wa Esperanca wanaokoa mpira huo
GOOOOOOOOOOO Dk 71, Msuva anaindikia Yanga bao safi kabisa kwa kichwa cha kurukia baada ya Mwashiuya kuingia na kupiga krosi safi la chini na Msuva anaruka kichwa cha chinichini na kuandika bao

Dk 65, Esperanca wanafanya shambulizi jingine kali lakini Yondani anakuwa mwepesi kutoka na kuokoa
Dk 58 hadi 63, Yanga wanawabana Waangola hao nusu uwanja. Hata hivyo wanaonekana kutokuwa na mipango mizuri katika umaliziaji

Dk 57, inaonekana wachezaji wa Esperanca wanaonekana kuwa wajanja kwa kupoteza muda mara kwa mara
Dk 52, Mwahiuya anapiga tena krosi nzuri lakini mabeki wa Esperanca wanakuwa makini na kuokoa

Dk 47, krosi nzuri ya Msuva lakini inakuwa ndefu inampita juu Tambwe
Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi, lakini bado inaonekana Yanga wanashindwa kuonyesha kama kweli watapata bao.

SUB: Yanga imefanya mabadiliko kwa kuwatoa Malimi Busungu na Salum Telela na nafasi zao kuchukuliwa na Geofrey Mwashiuya na Mbuyu Twite


MAPUMZIKO
Hadi mapumziko, mechi imemalizika bila timu yoyote bila kupata bao.

Yanga inalazimika kufanya kazi ya ziada ili kipindi cha pili ihakikisha inapata bao maana kama itashindwa litakuwa ni tatizo kwao katika mechi ya marudiano.
Kipindi cha kwanza kilikuwa kizuri zaidi kwa Yanga, hata hivyo ilipoteza nafasi nyingi za wazi zikiwemo zile za Malimi Busungu, Amissi Tambwe na Simon Msuva.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic