May 29, 2016

MAGURI
Timu ya soka ya taifa, Taifa Stars imepata sare ya bao 1-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars’ katika mechi ya kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.

Elius Maguri alikuwa wa kwanza kuifungia Taifa Stars bao katika dakika ya 33 akiunganisha krosi safi ya Juma Abdul.

Lakini dakika sita baadaye, Kenya wakasawazisha kupitia nahodha wao Victor Wanyama anayekipiga Southampton ya England ambaye alifunga kwa mkwaju wa penalti iliyolalamikwa kuwa siyo.

Pamoja na mabao hayo, Stars ilionekana kutawala zaidi kipindi cha pili mwisho na hata baada ya kuanza kipindi cha pili.

Hata hivyo, tatizo lilionekana ni kutokuwa na mipango imara katika safu ya ushambulizi.


Mechi hiyo ya Stars ni maandalizi ya kuivaa Misri mechi itakayochezwa Juni 4 jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic