May 29, 2016


Mbwana Samatta ameingoza KRC Genk kucheza play off za Europa League baada ya kuichapa Sporting Charleroi kwa mabao 5-1 katika mechi ya pili ya play off za Ubelgiji.

Ushindi huo umepatikana ukianza na Samatta kusababisha penalti iliyokwamishwa kimiani na Nikos Karelis katika dakika ya 20.

Dakika 7 baadaye Samatta akatupia kabla ya wapinzani wao kupata bao kupitia Jeremy Perbet na Sandy Walsh akaongeza la tatu kwa Genk.


Kipindi cha pili, Genk walipata mabao mengine mawili kupitia kwa Karelis huku wakiwa pungufu mara mbili baada ya wachezaji wao wawili kutolewa kwa kadi nyekundu. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV