Mabondia wa ngumi za kulipwa Mtanzania, Thomas Mshali ‘Simba asiyefugika’ na Muiran, Sajjad Mehrabi wametambiana kupasuana kesho Jumamosi katika pambano la kugombania Ubingwa wa Dunia UBO linalotarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar.
Sajjad ambaye ni mara yake ya pili kuja baada ya mwaka 2014 kucheza pambano lisilo kuwa la ubingwa dhidi ya Francis Cheka ambalo lilimalizika kwa sare kabla ya safari hii kurejea tena nchini kwa ajili ya kuchueza dhidi ya Mashali.
Mabondia hao kila mmoja ameonyesha nia ya kutaka kuibuka na ubingwa wa pambano hilo litakalo kuwa la raundi 12 kwa kutamkiana maneno ya vitisho vya kutaka kutoana roho ulingoni.
Mashali alisema hatarajii kuwaangusha Watanzania kesho kwa kuhakikisha anampa kichapo kikali mpinzani wake na ikiwezekana kumtoa roho ulingoni .
“Maandalizi makali niliyofanya nina uhakika yule Mwarabu hachomoki, yaani nife mimi au yeye lakini na kuhakikishia ubingwa utabaki Tanzania kwa sababu hapa achezi Mashali hapa inacheza Tanzania hivyo nitapambana kwa ajili ya Watanzania tu si zaidi ya hapo kwani lengo langu nataka akaisimulie kwao kuwa Mashali ni nani”.
Kwa upande wa Muiran, alisema kuwa: “Sioni sababu ya kushindwa kumchapa mpinzani wangu maana bado hayupo sawa kabisa mpaka aweze kunipiga mimi kwa sababu nimekuja tena hapa kwa ajili ya kuondoka na ushindi na siyo jambo lengine kwani raundi ndiyo zitaonyesha nani anastahili kuitwa bingwa”.
Licha ya pambano hilo mabondia wengine watakaopanda ulingoni ni Francis Miyeyusho ‘Chichi Mawe’ dhidi ya Frank Kiwarabi, Saleh Mkalekwa dhidi ya Joseph Onyango, wakati Ramadhani Shauri, Lulu Kayage na Nassibu Ramadhan hao watacheza na mabondia kutoka katika nchini Kenya, Malawi na Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment