CHEKA (KATIKATI) AKIWA NA SALEH ALLY NA JOHN JOSEPH. |
Bondia Francis Cheka, leo Jumamosi
anatarajia kupanda ulingoni kupigana na Mthailand, Kitschai Singwancha, kwenye
pambano la kimataifa la raundi kumi lisilo na ubingwa kwenye Ukumbi wa PTA
Sabasaba, Temeke jijini Dar.
Mabondia hao jana Ijumaa walipimwa uzito
ambapo Cheka alikuwa na uzito wa kilogramu 75.7 huku mpinzani wake akiwa na 75.
Cheka aliwaomba Watanzania kujitokeza
kwa wingi kushuhudia anavyomchapa Mthailand huyo kwani amejiandaa kwa ushindi
wa aina yoyote iwe kwa KO au pointi.
Kwa upande wake, Singwancha hakusita
kutamba kuibuka na ushindi huku akisema amekuja Tanzania kwa kazi moja tu ya
kumchapa Cheka.
Promota wa pambano hilo, Kaike Siraju,
alisema maandalizi yanaenda vizuri na ametolea ufafanuzi kuhusu baadhi ya
mabondia ambao walitarajiwa kupigana mapambano ya utangulizi.
“Kassim Ouma wa Marekani aliyetarajiwa
kupigana na Shaban Kaoneka, mpaka jana (juzi) mchana alikuwa hajatua nchini
licha ya kutumiwa tiketi mapema, pia Fred Nyakes aliyepaswa kupigana na Cosmas
Cheka, naye hatakuja kwani amegombana na meneja wake,” alisema Kaike. Pambano
hili limedhaminiwa na Global Publishers, Pepsi na Fore Plan Clinic.
0 COMMENTS:
Post a Comment