May 1, 2016


Mechi kati ya Manchester United dhidi ya Leicester City haikuwa mchezo, maana wengine wanataka ubingwa na wengine wanataka kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ndani ya Old Trafford, mechi hiyo imeisha kwa sare ya bao 1-1, lakini mtiti kati ya kiungo wa Man United, Marouane Fellaini dhidi ya beki wa kati wa Leicester City, Robert Huth umebaki kuwa gumzo.

Huth alitaka kumchanganya Fellaini na mara nyingi alikuwa akimvuta nywele.

Juhudi za Fellaini kuzuia shambulizi hilo la Huth kwa amani hazikuzaa matunda hadi alipoamua kufanya ile kazi yake anayosifika nayo.

Kupiga kiwiko, maarufu kama Pepsi. Huth akakaa chini kusikilizia maumivu.

Wachambuzi wanaeleza kwamba inawezekana Fellaini akaingia matatizoni na kufungiwa mechi tatu kama ile ishu ya Delle Alli wa Spurs. Lakini Huth aliyeanzisha vita kwa kuvuta nywele za mwenzake je?

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV