May 25, 2016


Hassan Kessy sasa ni mchezaji halali wa mabingwa Tanzania, Yanga.

Kama blogu hii ilivyokueleza kwamba leo atakwenda uwanjani wakati Yanga ikiivaa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kweli amefanya hivyo.

Amejitokeza kwenye Uwanja wa Taifa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Abeid Mziba ndiye alifanya kazi ya kumvalisha jezi ya Yanga kwa mara ya kwanza.

Mziba alimvalisha Kessy jezi hiyo wakati akiwa katika jukwaa la mashabiki wa Yanga na kuamsha shangwe kubwa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV