May 25, 2016


Mshambuliaji nyota wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa ametua nchini lakini moja kwa moja, akatinga Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam akiwa na jezi ya Yanga.

Ngassa ametua nchini jana, leo akafika uwanjani hapo kushuhudia mechi ya fainali Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya Azam FC akiwa amevaa na jezi ya Yanga.

Ngassa amewahi kuzichezea timu zote hizo, akianza na Yanga kabla ya kujiunga na Azam FC na baadaye akasonga Simba kabla ya kurejea Yanga.

Katika mechi hiyo, Yanga ilishinda kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kubeba Kombe la Shirikisho.

1 COMMENTS:

  1. Wachezaji wetu bado wana safari ndefu kujitambua kama professionals.Huyu ni mchezaji wa Free State anavaa fulana yenye nembo ya Yanga bila wasiwasi wowote.Hivi hao Free State wakimuona katika picha hiyo si ataadhibiwa kama yale ya kubusu nembo ya Yanga akiwa mchezaji wa Azam.Halafu Canavaro kapteni anakwenda kupokea kombe akiwa amevaa jezi ya Azam badala ya jezi ya Yanga!

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV