May 25, 2016


Hakuna mashabiki wenye furaha kama wa Yanga kwa msimu huu wa 2015-16.

Wamebeba ubingwa wa Tanzania Bara na leo Kombe la Shirikisho. Hii inawafanya wasichoke kufikisha ujumbe kwa watani wao hasa msemaji wa Simba, Haji Manara.

Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiingia na mabango yenye ujumbe mbalimbali, yakiwemo yale waliyolenga kumpa ujumbe Manara. Mojawapo, lilikuwa bango hili ambalo mashabiki wa Yanga waliingia nalo uwanjani wakati timu yao ikiivaa na kuitwanga Azam FC kwa mabao 3-1 na kufanikiwa kubeba Kombe la Shirikisho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV