May 11, 2016

Mashabiki wa West Ham United, walilishambulia basi la wachezaji wa Manchester United wakati wakiingia uwanjani Upton Park kuivaa timu yao katika mechi ya Ligi Kuu England.

Mechi hiyo iliisha kwa wenyeji kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, lakini Man United waliingia uwanjani wakiwa wamechelewa baada ya shambulizi hilo la mashabiki.

Mashabiki hao walirusha chupa na makopo ya vinywaji kuelekea katika basi hilo wakati likipita karibu yao chini ya ulinzi madhubuti wa polisi.

Ndani ya basi, wachezaji Man United walilazimika kulala chini katikati kwenye sehemu ya kupitia ili kuepuka kuumizwa!0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV