May 15, 2016

MANYIKA
Klabu ya Simba imeanza kusaka kipa mwingine mzoezi kwa ajili ya kukiimarisha msimu ujao.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Simba, zimeeleza tayari juhudi za kumnasa kipa mpya zimeanza.
“Kipa kweli anatafutwa, Manyika na Agbani pia watabaki. Lengo ni kutanua zaidi wigo katika nafasi ya ulinzi wakianzia na kipa.

“Kipa anayetafutwa anatakiwa kuwa wa humu Tanzania. Halafu Agbani yeye ataendelea kubaki,” kilieleza chanzo.


Kwa msimu wote, Simba zaidi imewatumia makipa wawili, Vicent Agbani raia wa Ivory Coast na Peter Manyika ambaye zaidi alidaka mechi za mwanzoni na sasa mwishoni amekuwa akipewa nafasi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV