May 15, 2016


MAJABVI
Wageni wenye uhakika wa kubaki katika kikosi cha Simba hadi sasa ni kiungo Justuce Majabvi na kipa Vicent Agbani.

Taarifa kutoka Simba zinasema, wawili hao ndiyo wameonekana kuuridhisha uongozi wa Simba pamoja na benchi la ufundi.

Lakini wengine watano waliobaki ambao ni Hamisi Kiiza, Juuko Murshid, Emiry Nimubona na Paul Kiongera wanaonekana hawana nafasi kabisa.

“Waliobaki pamoja na kwamba wako mwanzo walionyesha uwezo mzuri, lakini inaonekana hawana nafasi kabisa katika kikosi cha Simba msimu ujao.

“Wako ambao uwezo wao haukuwa kama ulivyotarajiwa, wengine ni majeruhi kila mara, wengine wanaonekana walikuwa tatizo ndani ya timu, hivyo uongozi utaachana nao,” kilieleza chanzo cha uhakika.

“Kweli Simba tumejifunza sana, wachezaji unawatunza, unawalipa mishahara, posho na hata fedha ya ziada. Mwisho wanageuka kuwa mwiba kwako.


“Tena wanageuka kuwa mwiba huku wanachama wakiamini hamfanyi kazi. Inaumiza sana, hao waache tu waende tutatafuta wengine. Simba ni kubwa kuliko mtu yoyote.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV