May 4, 2016Timu ya Uswahilini jana ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Michuano ya Mama Shija Cup baada ya kuichapa Wamang’ati mabao 3-2 katika mchezo mkali wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja Shule ya Msingi Mbagala Kingugi jijini Dar es Salaam, juzi.

Blog pekee ya SALEHJEMBE iliyokuwa uwanjani hapo kushuhudia Wamang’ati wakiwa wa kwanza kuandika bao lililofungwa na Mohammed Gazza dakika ya 27 ambaye awali alifunga bao lakini lilikataliwa.

Hata hivyo kibao kiliwageukia ambapo staa wa mchezo huo alikuwa ni Sulu Kasikasi ambaye aliifungia Uswahilini mabao yote katika dakika 32, 40 na 59 na kuiwezesha kuondoka na taji hilo. Bao jingine la Wamang’ati liliwekwa kimiani na Ramadhan Madebe dakika ya 39.

Kufuatia matokeo hayo Uswahilini wakatangazwa kuwa mabingwa wa michuano hiyo ambapo walipata zawadi ya kombe, jezi seti mbili na mipira miwili huku Wamang’ati ambao ni washindi wa pili wakipewa jezi seti mbili na mpira. Boda Boda wenyewe walikuwa washindi tatu na waliambulia jezi seti mbili na mpira mmoja.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV