Mshambuliaji nyota wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa ameendelea na mazoezi, safari hii akiwa amewekewa kocha maalum ambaye pia ni daktari.
Ngassa, Mtanzania pekee anayekipiga katika Ligi Kuu Afrika Kusini, amekuwa akifanya mazoezi gym na uwanjani.
“Mazoezi nafanya na mwalimu maalum, huyu pia ni daktari. Nakwenda gym tukiwa pamoja na hata nikienda uwanjani, mimi nafanya naye pembeni.
“Mazoezi nayofanya kila kitu ni maelekezo kutoka kwake,” alisema Ngassa alipozungumza na SALEHJEMBE moja kwa moja kutoka nchini Afrika Kusini.
Ngassa amefanyiwa upasuaji wa goti hali iliyomfanya akae nje kwa mapumziko kabla ya kurejea taratibu.
0 COMMENTS:
Post a Comment