May 28, 2016



MADRID

1. Vazquez-Wamepata
2. Wamepata-Marcelo
3.Wamepata-Bale
4.Wamepata-Ramos
5.Wamepata-Ronaldo


ATLETICO
1. Wamepata-Griezman
2. Wamepata- Gabi
3.Wamepata-Saul
4.Wamekosa-Juanfran
5.





MPIRA UKWISHAAAA SASA NI PENAAAAAAAAT

DK 120 zimekamilika, sasa ni zile 2 za nyongeza 
Dk 116 wanachofanya Atletico wanaonekana kama wanapoteza muda ili waende kwenye mikwaju ya penalti
Dk 115 Atletico wanamtoa Koke aliyekimbia zaidim ya Kilomita 14 wanamuingiza Thomas. 
Dk 108 Lucas Hernandez anaingia kuchukua nafasi ya beki wa kushoto Fillipe Louis ambaye anaonekana kuwa ameumia au ana tatizo na nyama za paja

Dk 107, bado mchezo mgumu, Madrid wanajitahidi kushambulia ingawa mashambulizi yao yanaonekana kutokuwa na nguvu kama yale ya Atletico wanaoshambuia kwa nadra
Dk 91 Mechi imeanza, inaonekana kila upande umepania kupata bao la mapema kumaliza mchezo

MPIRA UMEKWISHAAAA
Dk 87 Madrid ndiyo wanaonekana kushambulia zaidi lakini hakuna mashambulizi makali sana
Pia wanatakiwa kuwa makini kila wanapokwenda GOOOOOO Dk 79 Yannick Carrasco  anasawazisha bao safi kabisa la krosi hapa
Dk 78, Madrid wanafanya shambulizi kali labisa, kipa anaokoa mara mbili, Godin naye anaokoa na 
Dk 71, Kroos anakwenda kwenye benchi na Isco anaingia, hata hivyo inaonekana kama si sub sahihi lakini ndiyo kazi ya kocha Zidane
Dk 63 sasa, Atletico ndiyo wamashambulia zaidi, Madrid wameweka watu saba nyuma ya mpira kwa ajili ya kujilinda. Inabidi wawe makini, kwani kama watafungwa basi wanaweza kuongezwa
Dk 51 Danilo anaingia kuchua nafasi ya Carvajal ambaye ameumia, anatoka huku chozi likimtoka
Dk  47 Griezman anapiga penalti hapa, inagonga mtambaa wa panya na kurudi uwanjani, Madrid wanaokoa hapa
PENAAAAAAT DK 46  kipindi cha pili kimeanza kwa kasi na Atletico wanapata penalti hapa

MAPUMZIKO
Dk 44, Madrid wanaanza kupeleka mashambulizi mengi na Atletico wanapaswa kuwa makini pia
Dk 42 sasa, inaonekana Madrid wameamua kumaliza kipindi cha kwanza na bao hilo moja. Wengi wamerudi nyuma na wanafanya mashambulizi ya kushitukiza. Kidgo mabeki wao wamekuwa wakimsahau Griezman ambaye anaweza kuwadhuru
Dk 33 sasa, Atletico wanaonekana kuamka na kuanza kutawala sehemu ya katikati ya uwanja. Tayari wamefanyah amshambulizi matatu lakini bado hakuna kali sana
Dk 15, Ramos anaiandikia Madrid bao la kwanza kwa kuunganisha mpira wa kupara wa kichwa wa Bale

Sasa ni dakika ya 12, Madrid wamefanikiwa kufanya angalau mashambulizi matatu lakini bado hakuna bao.

Inaonekana Madrid wana kasi zaidi wanapoingia upande wa Atletico.
Kila upande umeanza mechi kwa kasi na kunaonekana kuna presha kubwa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic