May 19, 2016Mshambuliaji wa Genk  ya Ubelgiji, Mbwana Samatta ana imani kubwa ya kufanya vizuri kama tu atakuwa na afya njema.

Samatta amejiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu Ubelgiji akitokea TP Mazembe ya DR Congo aliyoiwezesha kubeba ubingwa wa Afrika.

“Naendelea vizuri ingawa ni kipindi kifupi, naona wananiamini pia nimezoea mazingira ya hapa,” alisema.

“Tumebakiza mechi mbili, nitarejea na mwisho ni maandalizi ya msimu ujao. Matumaini yangu ya kuwa kikosi cha kwanza ni makubwa lakini ni majaaliwa hasa nikiwa na afya njema,” alisema Samatta.

Tayari Samatta ameanza kuonyesha cheche zake katika mechi za ligi ya nchi hiyo akiwa na Genk kama kufunga mabao na kutoa pasi nzuri zinazozaa mabao.


Mtanzania huyo anazidi kuonekana ni msaada jambo ambalo litamsaidia kuaminika zaidi kwa kuwa ni mtendaji bora.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV