May 19, 2016Mabingwa wa Tanzania, Yanga wanatarajia kutua nchini kesho saa 9:30 wakirejea kutokea Angola.

Inaonekana mashabiki watajitokeza kwa wingi sana kwa kuwa imekuwa ni gumzo kubwa kwenye mitandao ya kijamii na wengi wakitaka kujua kikosi hicho kitawasili saa ngapi.

Yanga inatua nchini kwa kutumia ndege ya South African Airways wakipitia Johannesburg, Afrika Kusini ikiwa ni saa chache baada ya kuitoa Esperanca na kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Shirikisho.

Yanga sasa itacheza hatua ya makundi ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu ya Tanzania kushiriki michuano hiyo katika hatua ya makundi.


Tayari maandalizi ya mapokezi yameanza kufanyika na mashabiki kwa wingi wanatarajiwa kuipokea timu yao ambayo imefungw abao 1-0 lakini ikasonga mbele.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV