Uongozi wa klabu ya Simba umeamua kufanya mambo yake mengi kimyakimya kuhusiana na mabadiliko ndani ya kikosi chake.
Simba inataka kufanya mabadiliko makubwa ndani ya kikosi hicho na masuala mengi yamekuwa yakiangaliwa.
Moja ya mambo ambayo wamekuwa wakiangalia Simba ni kuhusiana na suala la wachezaji ambao watakuwa tayari kuitumikia Simba kwa dhati.
“Sisi kama viongozi hakika tulijitahidi sana, tulitoa kila kilichotakiwa ikiwezekana kwa wakati. Lakini miongoni mwa wachezaji walikuwa wasaliti wakubwa, wizi wa fadhila.
“Hivyo tumeamua kuangalia suala la kupata watu sahihi, tunajua kutakuwa na ugumu lakini lazima tujaribu kadiri ya uwezo wetu ili kilichotuumiza kisirudie tena,” alisema mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji alipozungumza na SALEHJEMBE na kuomba asitajwe jina.
“Sisi tunapambana, tunatoa fedha za mifukoni. Wachezaji wanazungumza na wengine na kutuuza. Wametumaliza sana, watu hawawezi kuamini lakini sisi tumeumia sana.”
Simba imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu baada ya mabingwa Yanga na Azam FC walioshika nafasi ya pili.
0 COMMENTS:
Post a Comment