Kocha Stewart Hall amerejea kwao Uingereza baada ya kumalizana na Azam FC.
Wakati anaondoka, alipata nafasi ya kuagana na mchezaji wake wa zamani, Mrisho Ngassa ambaye alikutana naye kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam.
Ngassa alikuwa anatokea Afrika Kusini ambako anaitumikia Free State Stars wakati Hall ndiyo alikuwa amemalizana na Azam FC.
Kocha huyo na Ngassa waliwahi kufanya kazi pamoja wakiwa Azam FC kabla ya Hall kuondoka na Ngassa akajiunga na Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment