Angalia taswira hizi 12 za gari aina ya Mercedes B-Class Electric Drive. Thamani yake ni pauni £32,670 (zaidi ya Sh million 103) kwa gari moja.
Tajiri Vichai Srivaddhanaprabha raia Thailand ameamua kutoa magari 30 aina hiyo kwa wachezaji na wale wa benchi la ufundi baada ya Leicester kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England.
Mercedes B-Class Electric Drive ni gari la kisasa linalotumia umeme badala ya mafuta.
Gari hilo huchajiwa kama ilivyo kwa simu, kawaida kuna vituo maalum kwa ajili ya kazi hiyo.
Vituo hivyo vinatumika kama sehemu ya kujazia mafuta kwa magari yanayotumia mafuta.
0 COMMENTS:
Post a Comment