May 5, 2016


Pamoja na mazoezi mengine, mshambuliaji nyota wa Free State Stars ya Afrika Kusini, Mrisho Ngassa amekuwa akijifua akifanyah mazoezi ya mchezo wa ngumi.

Mwanasoka huyo Mtanzania anayekipiga nchini Afrika Kusini, amekuwa akifanya mazoezi na mazoezi akiwa amewekewa kocha maalum ambaye pia ni daktari.

Ngassa amesema amekuwa akifanya mazoezi ya aina mbalimbali kuhakikisha anarejea fiti baada ya upasuaji wa goti alilofanyiwa.

“Nafanya mazoezi ya aina mbalimbali, kila kitu ni maelekezo yake kocha. Hivyo ngumi kama unavyoona ni sehemu ya mazoezi,” alisema.


Baada ya kutua katika kikosi hicho, Ngassa alipata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza. Lakini kuumia kulimuweka nje takribani mwezi kabla ya kufanyiwa upasuaji huo wa goti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV